Ufugaji Wa Ngombe

Mimi ni mfugaji, nitakushauri kufuga ngombe kwa mchakato ufuatao:
  • Ujenzi wa banda = Ths 500,000/=
  • Manunuzi ya Ngombe 5 x Tsh 900,000 = Tsh 4,500,000/=
  • (Ngombe utawanunua wakiwa na mimba ya miezi 6)
  • Kuwahudumia ng'ombe kwa miezi mitatu kabla ya production = Tsh 1,500,000/=
  • (inahusisha mshahara kwa wafanyakazi wawil + chakula + madawa)

Jumla = Tsh 6,500,000/=


 


Baada ya Miezi 3;

UZALISHAJI:

Ngombe hawa watakuwa wakitoa maziwa si pungufu ya lita 5 kwa asubuhi na jioni kwa kila ng'ombe. Hivyo uzalishaji kwa siku utakuwa lita 10 kwa siku kwa ng'ombe.

MAPATO

Lita 10 x Ng'ombe 5 = lita 50 kwa siku x Tsh 1000 (bei ninayouza mimi hapa) = Tsh 50,000 kwa siku
Mapato kwa mwezi = Tsh 50,000 x 30 = 1,500,000/=

Gharama za uendeshaji kwa mwezi = Tsh 600,000/=

Faida = Tsh 900,000/= kwa mwezi

BAADA YA MIAKA 5:

Kumbuka ng'ombe huzaa kila mwaka hivyo basi baada ya miaka mitano utakuwa na ng'ombe wasiopungua 25. Kipato chako kwa mwezi unaweza kufikia si pungufu Tsh 18,000,000 endapo utakuwa na ngombe jike 20 kati ya hao 25.
Ufugaji Wa Ngombe Ufugaji Wa Ngombe Reviewed by Unknown on 1:50:00 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.