Kuku wa kienyeji (Pure) - Biashara kichaa isiyo na tija

Kumekuwa na upotoshaji kwa baadhi wa watu wanaojiita wataalamu wa ujasiriamali, hasa wanaofanya shughuli za ufugaji kwa maandiko ya whatsapp bila kuwa na hata kuku mmoja bandani.

Nimesukumwa kuandika bandiko hili hapa kutokana na jumbe mbali mbali za uufugaji wa kimtandao unaoshawishi vijana kuwa watatajirika mapema kwa shughuli za ufugaji kwa kuanza na kuku wa kienyeji kumi na moja na kuweza kupata Zaidi ya kuku miatatu ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa uzalishaji. Hoja yao inaweza kuwa sahihi, ila ningependa kusisitiza mafanikio katika ufugaji hayapo katika idadi ya kuku unayomiki, bali ni namna ulivyoweza kumanage biashara ya ufugaji.

Hoja yangu leo hapa ni kwamba, Biashara ya kuku wa kienyeji hailipi na nikupoteza muda wako. Na nitatetea hoja yangu kwa mifano hai na uzoefu wangu katika ufugaji.

Biashara ya Mayai. (idadi isiyo na tija kibiashara)

Kwa asili ya kuku wa kienyeji,huwa wanatabia ya utagaji wa mayai 7-10 na mara nyingi ni siku kwa siku 10 mfululizo, utamiaji -siku 21, na uleaji wa vifaranga - siku 50-60. Hii inampelekea kwa kuku mmoja kuweza kutaga wastani wa mayai 35-50 kwa mwaka kwani anapoteza muda mwingi kwa shughuli za utamiaji na malezi ya vifaranga badala ya kutaga. Idadi hii ya mayai haina tija kibiashara kwani kuku mmoja anaweza kukuzalishia tray 1 mpka mbili kasoro pekee kwa mwaka ambayo kwa bei ya soko si Zaidi ya shilingi za kitanzania 20,000 tu kwa mwaka.

Changamoto kwenye soko la mayai ya kienyeji. (Uhifadhi wa mayai)

Mayai ya kienyeji ni kati ya bidhaa ngumu Zaidi kuhifadhika. Ikumbukwe kuwa tofauti na mayai ya kisasa, mayai ya kienyeji huwa yamerutubishwa na majogoo. Hivyo kuharibika ndani ya muda ya week moja au pungufu kama hayatatuzwa katika mazingira salama kwaajili ya utunzaji. Kipindi cha joto kali, mayai haya huanza kujitenenezea kifaranga au mishipa ya damu ambayo baada ya muda mfupi hugeuka viza na kutofaa kwa matumizi tena.

Kwa uzoefu wangu binafsi, nilianza kusambaza mayai ya kienyeji kwenye supermarkets miaka mitatu iliyopita. Nilipata changamoto kubwa sana ya kubadilisha mayai mara kwa mara kwani mteja akichukua yai viza ni kumpoteza kabisa. Hii ni changamoto ya kwanza ambayo mpaka sasa bado inasumbua wafugaji wengi.

Bei juu kwa mayai ya kienyeji

Gharama za mayai husika, bei ya mayai ya kienyeji iko juu ukilinganisha na gharama za mayai ya kuku wa kisasa. Soko kubwa la mayai ni pamoja na vibanda vya chips, migahawa na hoteli. hawa wanauhitaji mkubwa sana wa mayai na soko liko juu muda wote wa mwaka.

Soko la mayai ya kienyeji lipo Zaidi kwenye households(soko la familia) hasa kwa vigezo vya kuzingatia afya zaidi. Soko hili la familia sio kubwa, ni soko dogo na mara nyingi hutumia tray moja kwa kipindi cha wiki mbili au Zaidi. Kwa mzalishaji mkubwa wa mayai ya kienyeji ni lazma awe na soko la familia pana Zaidi kuweza kupata faida ndogo, nasema faida ndogo maana ili kuzalisha mayai tray kumi (mayai 300) kwa siku, utahitaji Zaidi ya matetea 700 mpaka 1000 ya kienyeji pure. idadi ambayo ni kubwa kuliko idadi ya mayai yanayopatikana.

Biashara ya Nyama

Na declare interest, mimi pia ni msambazaji wa nyama ya kuku wa kienyeji, hivyo naongea kwa uzoefu, na niko tayari kukosolewa. Pamoja na kufugwa katika misingi ya kijani (organic rearing), iyo pekee haitoshi kumpa thamani inayostahili huyu kuku sokoni.

Thamani ya kuku sokoni ni uzito alio nao, organic component ni jambo la ziada lililo muhimu pia. tunavyo jadili bei ya soko ya kuku huyu ni lazma tumliganishe na gharama za bidhaa pinzani zilizoko sokoni. Haitawezekana kumuuza kuku mwenye kilo moja au pungufu kwa bei ambayo tunashawishiana humu ya 15,000-20,000 wakati bidhaa pinzani (nyama nyeupe) kama samaki sato toka mwanza wanauzwakwa 7,500 kwa kilo, au kitimoto, nyama ya ngombe ambazo nazo kilo ni 7,500-8,000.

Hivyo basi, hoja yangu hapa ni uzito wa kuku husika. Ukiachana na jamii chache za kuku wa kienyeji (kuchi etc) wenye uzito mzuri, majority ya kuku pure wa asili/kienyeji kwa majogoo huwa na pungufu ya kilo moja na nusu. Kumbuka uzito wa kuku hawa sio kwasababu ya malisho duni, laah hasha, bali ni kutokana na vinasaba (genes) vyao kuwafanya kuwa na maumbo madogo madogo. kwa kuku wa aina hii, sitegemei mfugaji kama atafanikiwa kuwapeleka sokoni na kuweza kupata bei nzuri toka kwa mlaji wa mwisho.

Nini kifanyike?

Ili ufugaji uwe wenye tija kibiashara ufanyike, ni lazma wafugaji tuamke na kuachana na ufugaji wa kuku hawa asilia kwani hawana tija. Nikisema hivi simaanishi watu waache kufuga, hapana, ila wafuge aina /breeds za kuku zenye tija kibiashara. Kuku pekee unaoweza kuwafuga kwa mbinu za kienyeji na bado wakakuletea mfugaji faida nzuri kibiashara, ni kuku aina ya chotara (cross breeds). Hii ni aina ya kuku wenye sifa zote za ukienyeji kwa misingi ya mbinu zao za kuwafuga pamoja na namna walivyo nauwezo wa kuhimili mazingira hasa ya vijijini.

Kuna aina mbalimbali ya kuku hawa ikiwamo Black/ white australorps, kroiller, Rhodes island red, red hamshire, Sussex etc. Hawa ni kuku ambao wanaserve purpose zote za mayai na za nyama. Mfano kuku aina ya black/white australorps wao wanauwezo wa kutaga mpaka mayai 250 kwa mwaka, tofauti na wa kienyeji, mayai ya kuku hawa huwa makubwa na yenye kasha jeupe na kiini cha njano kama utawafuga kwenye mazingira na mbinu asilia (za kienyeji).

Ukilinganisha uwezo wa utagaji wa kuku hawa utagundua utagaji wao ni Zaidi ya asilimia 500% ukilinganisha na ule wa kienyeji pure. Idadi hii ya mayai toka kwa kuku mmoja kwa mwaka, anaweza kumwezesha mfugaji kuzalisha mayai kwa wingi na kushusha Zaidi bei ya mazao yake (mayai) kuwa chini kuweza kuliteka soko kwa urahisi Zaidi. Kumbuka, bei ya juu ya mayai ya kienyeji ni kwaajili ya kulipia gharama kubwa za utunzaji wa kuku huyu ilihali utagaji wake ni hafifu.

Pili, kuku hawa wana nyama nyingi Zaidi kuliko hawa wa kienyeji kwa majogoo hufikia mpaka uzito wa kilo 3-3.5. huku matetea hufikia kilo 2-2.5 na huwa na nyama nzuri, iliyokomaa vyema na yenye ladha. kwa uzito huu kwa majogoo, kuku hawa uuzwa kwa bei ya 20,000 - 25,000 wakiwa hai. bei ambayoni kwa mujibu wa bei ya soko kwa makadirio ya shilingi 8,000 kwa kilo kwa nyama nyeupe.

Mapungufu

Pamoja na ubora wa kuku hawa katika ufugaji wa kibiashara, kuku hawa pia wanachangamoto mbali mbali ikiwemo kutokuwa na uwezo wa kutamia. Pamoja na hii kuwa changamoto pia ni fursa kwani kwa yeye kutotamia kunamwongezea nafasi ya yeye kuendelea kutaga mara nyingi Zaidi bila kupumzika. Hivyo changamoto hii ni faida kwa mfugaji anaelenga kufuga kwa tija. Kwa vile mayai haya huwa yamerutubishwa na majogoo, nirahisi kwa mfugaji kuongeza idadi ya kuku kwa kupitia kutotolesha kwa mshine za kuangulia vifaranga au kumpa kuku mwingine ayatamie kwa niaba.


Neno la kufungia:


“ I think I touched a raw nerve when I said farming is NOT cool! I believe farming takes a lot of HARD work and dedication. Lets not lie to the youth that they'll become instant millionaires when they get into farming. It becomes "cool" once you master the trade......” caleb

Ufugaji unalipa ukiweza kuibudu biashara ya ufugaji,


Kwa ushauri Zaidi kuhusu shughuli za ufugaji, tuwasiliane kwa namba 0755815174. pia pata fursa kusoma ya Makala mbali na utaalamu kutoka kwenye mtandao wetu www.backyard.co.tz

Nimejaribu kuattach picha za baadhi ya kuku bora wanaofaakufugwa kienyeji na wakaleta tija kibiashara hapa chini. Neno langu si sharia, nakaribisha Michango

WP_20150805_049 - Copy.jpg
WP_20151026_006.jpg
WP_20151101_001.jpg
WP_20151118_002.jpg
WP_20151229_003.jpg
 
Kuku wa kienyeji (Pure) - Biashara kichaa isiyo na tija Kuku wa kienyeji (Pure) - Biashara kichaa isiyo na tija Reviewed by Unknown on 11:32:00 PM Rating: 5

17 comments:

  1. nimekuelewa vizuri sana.unapatikana wapi?

    ReplyDelete
  2. Wewe Ni mpuuzi sana unataka kuwapumbaza watu ili waje kununua hao kuku wako .nonsense sana kuku wa kienyeji wamenipa zaidi ya milioni 70 ndani ya miaka 2 .kwenda kabisa .maskini wa fikra na mbinafsi sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. kaka naomba mawasiliano yako, mimi napatikana kwa 0713312861

      Delete
    2. Je naweza kupata mawasiliano yako? Mimi napatikana kwa namba 0744874521

      Delete
    3. Naomba namba zko. 062255795429

      Delete
  3. Wewe Ni mvivu na research yako ni ya kitoto sana njoo uone kuku wa kienyeji kwangu .rabbish sana .watanzania Kama Hawa hawanapaswa wafe kabisa .

    ReplyDelete
  4. majadiliano ya kutafuta maendeleo yasigeuzwe matusi au kashfa kutokana na mawazo aliyoyatoa mtu. toa maoni yako kwa jinsi unavyojua tu na si vinginevyo, la sivyo mijadala yetu haiwezi kuwa na tija/mafunzo kwa yeyote.

    ReplyDelete
  5. Kaka nimekuelewa sana sana ntakutafuta unipe ushauli niianze hii biashara ya ufugaji wa hao kuku , binafsi umenifungua

    ReplyDelete
  6. Kaka ameongea ukweli wake tusimtukane ila ukiangalia kuku wa kienyeji kwa kweli wanachukua muda mrefu kuanza kutaga pia hawana uzito mkubwa kama chotara

    ReplyDelete
  7. ni vyema tubishane kwa hoja si matusi au..

    ReplyDelete
  8. Mm nimemwelewa Sana cha mcngi Ni kutafakari Na kuchukua hatua

    ReplyDelete
  9. Mimi nipo Zanzibar sisemi wakienyej hawanufaiishi wananufaisha ila mpaka inufaike ni mproses ndefu mfo.mim nauza mayai ya kuku wa kienyeji my no.0777345317 ila bado wateja ni changamoto sana ndugu zangu

    ReplyDelete
  10. Nimepitia comment ila Bado sijapat jibu nifuge kuku wa had na gani😔

    ReplyDelete
  11. Kwani ailicho kiongea mwandishi Wa hii makala amekosea Nini!au ameharibu biashara zenu mbona mnamtukana bila sababu, tubishane kwa hoja ndio maendeleo

    ReplyDelete
  12. Kwa upande wangu ngependa kumpongeza mwandishi kwa alichoandika coz *its very true* kutokana na experience kwenye ufugaji wangu ....mtu kama huyu anahitaji pongezi ktk jamii maana wengi wamekua wakipotosha watu....kiufupi kile alichosema ni ukweli mtupu.....mm nimefuga kroila na kienyeji pure na layers kwa wakat mmoja.... nataka nitoe summary tu kwa uhalisia wangu kwa upande wa hao chotara na kienyeji ....kwa chotara baada ya miez 5 jogoo alikua na kilo 3 na wengine mpaka 3.5 nilianza kiwauza kwa bei ya elfu25 majike nilitunza kwa ajili ya mayai ...kuku wa kienyeji alikua bado mno walianza kutetea miez6 around miezi7 nkaanza kuokota mayai lakini uzito wake na umbile lake alikua bado kuuzwa sokoni wakataga mpaka kufika miezi 9/10 ndipo nilianza kuuza kwa bei ya elfu10 ...sasa ki uhalisia huyu kuku wa kienyeji nilimuhudumia kwa sh elfu1 kwa mwezi kweli? Hii ni hasara niliwauza wote nkawatoa kabisa na sina mpango nao tena msaada walionipa hao kuku ni kuatamia mayai kwa ajiri ya vifaranga wangu wa layers na chotara lakini ukisema ni kwaajili ya mayai na kuuza kwa nyama hamna tija ..wanakua na faida ukiwafuga free range sasa una kuku 300 unaweza kuwafuga free kweli tuwe na uhalisia tu kulingana na jamii tunamoishi...mimi wangu nilifuga indoor na hiyo ndo ilikua a tathmini kwa upande wa kienyeji kwa nyama....

    ReplyDelete

Powered by Blogger.