Hapo zamani kulikuwa na binti mmoja alikuwa anamlalamikia babake juu ya
maisha magumu.Binafsi yeye hakujua ni siku gani atafanikiwa na alikuwa
ameshakata tamaa katka kupambana na kuhangaika muda wote, kwa kuwa kila
alipotatua changamoto moja nyingine kubwa zaidi inaibuka.Babake alikuwa
mpishi, Siku moja akamuita jikoni, akainjika sufuria tatu zenye maji
kwenye jiko la moto mkali.
Pindi sufuria zilipopata moto maji yalichemka. Akachukua viazi akaweka kwenye sufuria A, na Mayai kwenye sufuria B na nafaka za kahawa kwenye sufuria C.Wakaketi kimya bila hata mmoja wao kumsemesha mwenzie.Binti alikuwa na utulivu na hamu ya kujua nini kitatokea.
Baada ya kama dakika ishirini hivi, baba alizima jiko na kuipua viazi na kuviweka kwenye bakuli na mayai vivyo hivyo na baadae akaipua Yale maji ya nafaka za kahawa na kuyamimina kwenye kikombe.
Akamtizama bintiye akamwambia umeona nini? La hasha! binti akamjibu kwa bashasha ni viazi,mayai na kahawa. Mzee akamjibu naam ndivyo hivyo..Tena akamuuliza naomba ushike kiazi, binti akashika akaona kiazi ni laini, chukua na yai pia na ulivunje binti akafanya hivyo nakuona yai ni gumu baada ya kuchemka kwenye maji ya moto na mwisho Mzee akamwabia aonje ile kahawa kwenye kikombe..naam binti akatabasamu baada ya kuionja nakusema ni nzuri sana.
Baba akauliza hayo yote yana maanisha nini?
Baba alifafanua tumeona viazi,Mayai na nafaka za kahawa vyote vimekabiliwa na joto Kali la maji yaliyochemka kwenye sufuria na tumeshuhudia kila kimoja wapo kimelipokea joto hilo tofauti. Viazi vilikuwa vigumu baada ya kukabiliwa na joto vimekuwa laini, mayai yalikuwa laini lakini baada ya joto Kali yamekuwa magumu na nafaka baada ya kuwekwa kwenye maji zimetengeneza ladha nzuri na tamu.
Baba aliuza tena, wewe ni yupi hapo?
Baba alifafanua, pindi tunapokabiliwa na changamoto tunakuwa na hali gani? Viazi,yai au nafaka za kahawa?
Moral: In life, things happen around us,things happen to us, but the only things that truly matters is how you choose to react to it and what you make out of it.
Life is all about learning, adopting and converting all the struggle that we experience into something positive.
#shabaha #tafsiriyamtandao + #mawazohuru
Struggle of life - Elimika na Masimulizi Ep 4
Reviewed by Unknown
on
2:02:00 AM
Rating:
No comments: