Mfumo Wa Kutotoresha Vifaranga Kwa Kutumia Mafuta Ya Taa
Baada ya Rais wa Jamuhuri Ya Muungano Tanzania kutangaza ya kwamba katika katika uongozi wake, itakuwa ni serikali ya viwanda, watu wengi walijiuliza ni kivipi, inawezakana kuwa hivyo?
Hata mimi ni miongoni mwa watu hao, ila baada ya kufanya uchunguzi mtu anapozungumzia viwanda maana yake nini? basi nikaja kupata majibu ya kina kuwa Tanzania ya viwanda inawezekana kabisa.
Ngoja nikushirikishe juu ya utafiti wangu. Unapozungumzia Tanzania ya viwanda katika fikra za watu ni kwamba watu wengi wanawaza katika picha kubwa sana, ukiwaza katika misingi hiyo utakuja na jibu ya kwamba haiwezekani kabisa.
Lakini endapo utawaza Tanzania ya viwanda katika picha ndogo pia inawezekana kabisa. Katika kuwaza katika picha ndogo utakuja kugundua ya kwamba nchi ya Tanzania ina viwanda vidogo vidogo vingi sana ambavyo endapo vitaweza kutambuliwa vinaweza kuifanya Tanzania kuwa katika sura mpya ya viwanda zaidi.
Ukichunguza kwa kina hapa nchini hata yule mtu anayeshona nguo, anayepasua mbao, anafanya uhunzi wa kutengeneza majiko,sufuria, vijiko, kufyatua tofari vyote ni viwanda ila kwa sababu hatuvipi thamani vitu hivyo tunaona ni vitu vya kawaida sana.
John Haule kulia akiwa na Afisa Mipango Benson |
Hata hivyo endapo vitachukuliwa kama ni viwanda wapo baadhi ya watu kutoka mataifa mbalimbali wataagiza vitu hivyo kutoka hapa nchini. "Usipeleke hirizi sokoni ila kuwa wa mbunifu kwa jambo ambolo unalifanya"
Huu ni msemo ambao unatupa hamasa kama kweli tunahitaji Tanzania ya viwanda, kama tunahitaji ubunifu wa vitu vyetu na sio kuiga vitu ambavyo vimekwisha tengenezwa.
Katika harakati za kutafuta ukweli wa jambo hilo, niliweza kukutana na John haule ambaye alinishangaza juu ya ubunifu wake. Yeye ameweza kutengeneza mashine ya kutotoresha vifaranga vya kuku ambayo inatumia mafuta ya taa.
Katika harakati za kutafuta ukweli wa jambo hilo, niliweza kukutana na John haule ambaye alinishangaza juu ya ubunifu wake. Yeye ameweza kutengeneza mashine ya kutotoresha vifaranga vya kuku ambayo inatumia mafuta ya taa.
Mashine hizi zipo za aina tofauti kulingana na mahitaji ya mteja, mashine Hii ipo ambayo ina uwezo wa kutotolesha idadi ya vifaranga kuanzia 30 na kuendelea. Mashine hii inauwezo wa kutumika mahali popote pale amabo mfugaji atahitaji kufanya shughuli zake.
Muonekano wa mashine hii;
Mwonekano wa nje wa mashine |
Ina nafasi pana kwa ajili ya kuweka mayai kwa ajili ya kutotolesha vifaranga. Upande wa ndani ina taa za mafuta ya taa ambayo itawaka kipindi chochote cha kukutolesha vifaranga, pia mashine hii ina thermometer ambayo kazi yake ni kupima joto litakalokuwepo pindi Mayai yanafanya kazi ya kutaka kujitotolesha
Namna ya kuchagua mayai kwa ajili ya kuweka kwenye mashine hiyo.
1.Hakikisha yai au mayai ambayo unayaweka hayazidi siku 12 tangu kutotolewa.
2. Hakikisha yai ambalo halijatagwa na kuku mzee.
3. Pia hakikisha mayai hayapatwa na msukosuko mingi kama kupakia kwenye baiskeli.
4. Hakikisha kwamba mayai ambayo unaweka kwenye mashine hii yanakuwa sio mayai ambayo machafu.
5.Hakikisha kuweka mayai ambayo umekusudia kuweka maana endapo utaweka hata yai la nyoka utalikuta baada ya kutotoleshwa utakuta hata watoto wa nyoka.
Namna ya kuitumia mashine.
Hakikisha kuwa taa inawaka muda wowote, wa kuatamia kwa mayai. Pia pindi mafuta ya taa yakiisha unaongeza.
5.Hakikisha kuweka mayai ambayo umekusudia kuweka maana endapo utaweka hata yai la nyoka utalikuta baada ya kutotoleshwa utakuta hata watoto wa nyoka.
Namna ya kuitumia mashine.
Hakikisha kuwa taa inawaka muda wowote, wa kuatamia kwa mayai. Pia pindi mafuta ya taa yakiisha unaongeza.
Hakikisha ya kwamba kila baada ya masaa 6 unachezea mayai kama ambavyo kuku hufanya.
Hakikisha pia unakuwa unaangalia joto ambalo linakuwa ndani ya mashine hiyo kupitia thermometer hiyo. Joto kwenye thermometer hiyo linakuwa kati ya 37. Maana likizidi au likipungua linakuwa na madhara kwa mayai.
Baada ya hapo vifaranga hivyo kutolewa utaviacha ndani ya mashine hiyo ambayo inatumia taa kwa siku mbili kisha unavitoa na kuvipeleka katika banda la kufugia vifaranga ( bluda) kisha unavianzisha vifaranga hivyo chakula cha mwanzo cha vifaranga (stata )
Baada ya hapo vifaranga hivyo kutolewa utaviacha ndani ya mashine hiyo ambayo inatumia taa kwa siku mbili kisha unavitoa na kuvipeleka katika banda la kufugia vifaranga ( bluda) kisha unavianzisha vifaranga hivyo chakula cha mwanzo cha vifaranga (stata )
Kutokana na takwimu kutoka bodi ya takwimu ya mwaka 2012 zaidi ya kaya milioni 2.3 zinafanya ufugaji ambao ndio chanzo cha watu wengi kupata kipato.
Hata hivyo takwimu ya bodi hiyo inasema milioni 35.5 ni idadi ya kuku wa asili, milioni 24.5 ni idadi ya kuku wa kisasa ambayo inatupa jumla ya milioni 60.1.
Pia takwimu hizo zinaonesha ya kwamba kwa hapa Tanzania baadhi ya mikoa ambayo inaongoza katika ufugaji ni Shinyanga, Mbeya, Mwanza , Tabora, Morogoro, Iringa, Simiyu,Tanga na sehemu zinginezo pia inakadiliwa kuwa kilo 6.8 za nyama huliwa kwa mwaka.
Uzuri Wa mashine hii ni kwamba unaweza kutengeneza kipato kingi na kuacha kulalamika suala la umaskini au ajira kwa ujumla wewe kijana mwenzangu.
Hii ni fursa tosha ya kufanya ufanikiwe zaidi leo hii endapo utaamua kuifanya. Pia kwa kuwa ni fursa ambayo inaenda sambamba na Tanzania ya viwanda hivyo inakujali sana kwa namna moja ama nyingine katika kuondokana na umaskini.
Pia uzuri mwingine wa kifaa hiki ni kwamba inabana matumizi ya umeme na kama ni kijijini ambako ndiko kwenye idadi kubwa ya watu.
Pia tumshukuru Mtanzania mwenzetu kwa mara nyingine tena John Haule. Kwani amekuwa mbunifu kuweza kuleta njia ya kuondokana na umaskini kwani ni zamu yetu kuwa wazalishaji na mataifa ya nje kuwa watumiaji Wa bidhaa zetu.
Kuna mataifa ambayo naamini ya kwamba ni zamu yao kutumia bidhaa zetu.
Unaweza ukawasiliana nami afisa mipango, ikiwa unapenda kujua zaidi kuhusu mashine hizi, nami nitakuunganisha na mtaalamu wetu John Haule.
Mfumo Wa Kutotoresha Vifaranga Kwa Kutumia Mafuta Ya Taa
Reviewed by Unknown
on
4:14:00 PM
Rating: 5
No comments: